ULIMWENGU WETU UMETAWALIWA NA BARIDI KALI SANA
Kuna mtu aliuliza swali kwanini wakati wa Usiku huwa kuna baridi katika maeneo Mengi ya dunia yetu ?
Kwanza kabisa inatakiwa ufahamu ulimwengu wetu ni mkubwa sana Ulimwengu uliotawaliwa na giza kubwa sana yote ni kutokana maeneo mengi ya ulimwengu wetu hayapati chanzo cha nishati mwanga au tuseme mwanga haufiki katika maeneo mengi sana ya ulimwengu wetu
Kama tunavyofahamu kuwa Nyota ndio chanzo kikubwa sana kinachozalisha Joto huko anga za mbali sasa kutokuwepo na chanzo hicho katika maeneo mbalimbali huko anga za mbali au kutokufika kwa chanzo hicho katika maeneo mbalimbali basi husababisha kutokuwepo na Joto kabisa katika maeneo mengi huko anga za mbali hivyo kama tunavyofahamu Joto likitoweka basi baridi huja na kupelekea hali ya ubarafu kutokea
Kama tunavyofahamu Dunia yetu huwa imetenganisha na sehemu kuu mbili kuna ule upande wa giza na kuna ule upande unaotazama Jua hivyo upande unaotizama Jua huwa na Joto kwasababu huwa unafikiwa na chanzo cha Joto na huu upande wa pili hukosa chanzo cha Joto hivyo huanza kuendana na mazingira yanayopatikana katika eneo hili lisilofikiwa na Joto linalozalishwa na Jua
Ngoja nikupe mfano kipindi cha Apollo 13 wakati wanaanga walivyokuwa katika safari ya kuelekea Mwezini walipokuwa wakikaribia mwezini kulitokea Hitilafu katika mitungo na mifumo ya hewa na uzalishaji wa Joto ndani ya chombo hicho walichokuwa wakisafiria nacho
Hivyo wanaanga walipitia wakati mgumu sana baada ya kuwa katika ule upande ambapo Mwanga wa Jua haufiki tuseme walivyokuwa katikati ya Dunia na Mwezi hivyo kupelekea baridi kuzidi mpaka kusababisha barafu kuanza kujiunda ndani ya chombo chao
✔️ Kama itatokea dunia ikashindwa kuzunguka basi kuna baadhi ya upande wa dunia maisha yatakuwa ni ya tabu sana kwasababu bahari zitaganda na baridi kali sana litatokea kwakuwa upande mmoja wa dunia utakosa chanzo cha Joto.
Mwandishi : KALISTI J FELIX
Mawasiliano: 0672241912
Comments
Post a Comment