πŒπ€π„π‹π„π™πŽ π˜π€ 𝐂𝐀𝐅 𝐓𝐅𝐅 π–π€π‰πˆπ“π€π…π€πŠπ€π‘πˆ



➪Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, limetoa maelekezo kwa vyama wanachama wake ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwamba mwisho wa kuwasilisha majina ya klabu na wachezaji wao kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Afrika msimu ujao ni Juni 30, 2022. 

➪Baada ya hapo hakutakuwa na klabu itakayopokewa na wala wachezaji watakaoruhusiwa kushiriki mashindano ya Afrika.

➪Hii ina maana kwamba Tanzania inaweza kukosa wawakilishi wa mashindano ya Afrika msimu ujao kama msimu wake wa soka hautakamilika ndani ya muda huo. 

➪Hadi sasa kwa mujibu wa ratiba ya TFF, msimu wa Tanzania utakamilika Julai 2 kwa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

➪Yaani fainali ya Shirikisho ambayo itamtoa mshiriki wa Kombe la Shirikisho la Afrika itafanyika nje ya tarehe rasmi ya CAF. 

➪Hii ni changamoto kubwa INASIKITISHA..😬

#Powered by:-
KAJO MEDIA PRODUCTIONS

Comments

Popular posts from this blog

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2021

MADA MEZANI on KAJO ONLINE RADIO