MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA MAKONDA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mkoani Dar es Salaam imetupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na mapungufu ya kisheria.
Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 3,2021 na Hakimu Allon Lyamuya.
#KAJOMNJELUBLOGUPDATES
Kesi ya maombi ya jinai No 7 ya 2021 iliyokua inamkabili DPP, DCI na Mkuu wa mkoa Mstaafu Wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Imetupiliwa mbali na mahakama ya hakimu mkaazi ya kinondoni leo tarehe 3/11/2021 kwa kukosa mashiko ya kisheria.
Hakimu mkaazi wa mahakama hiyo A. Lyamuya alifikia uamuzi huo baada ya kubainika kwa makosa yasio tibika kwenye nyaraka za mleta maombi ya kuwashitaki DPP, DCI na Paul Makonda.
Awali Mwanasheria wa mleta Maombi H. Mwaisepu alioiomba mahakama kuondoa hati yake maombi ili arekebishe makosa hayo, lakini hakuweza kubainisha ni kwa kifungu kipi cha sheria anafanya maombi hayo. Hivyo kusababisha kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Comments
Post a Comment