JE, WAJUA KITU BINADAMU ANACHOPENDA KULIKO VYOTE DUNIANI?
Watu wanaweza wakawa na majibu tofauti mengi kuhusiana na swali hili kwamba, ni kitu gani ambacho wanadamu hupenda kuwa nacho kuliko kitu kingine chochote kile hapa chini ya jua. Simaanishi ile kanuni maarufu ya “ Maslow’s hierarchy of needs” ya hatua za mahitaji ya binadamu, kwani ingelikuwa ni hiyo basi tungelisema binadamu anahitaji zaidi chakula na malazi ili aweze kuishi. Kwa mtazamo wa wengi jibu linaweza likawa ni moja kati ya vitu hivi vifuatayo( vimetajwa baadhi tu ) kabla hatujaangalia jibu sahihi ni lipi la ni kitu gani binadamu anachopenda zaidi kuliko vitu vingine vyote hapa Duniani. PESA. Bila shaka yeyote, idadi kubwa ya watu ni lazima watajibu kwamba, kile wanachopenda zaidi maishani mwao wawe nacho ni PESA, au kwa maneno mengine wanapenda kuwa na utajiri utakaowawezesha kununua kila kitu wakipendacho. Binafsi siwezi nikabisha hilo ingawa sina hakika ikiwa pesa ina uwezo wa kununua kila kitu hapa duniani. KAZI NZURI. Wengine watataja, wangependa kuwa na ajira nzuri