MAANA YA SAIKOLOJIA NA NAFASI YAKE KATIKA JAMII -2
Ijumaa, March 25, 2022 Mwandishi wa makala hii ni Sir FELIX, KALISTI J ni Mwanafunzi wa Shahada ya Elimu katika Saikolojia(BED-PSYCHOLOGY) kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM). Anapatikana kwa:- Barua pepe: kajomnjelu@gmail.com Simu: 0672241912/ 0629835302 Tuliona katika makala iliyopita maana ya saikolojia na kuhitimisha kwamba kinachotazamwa zaidi katika saikolojia ni tabia. Kwa hakika matatizo mengi yanayoikabili jamii yetu chanzo chake ni tabia. Tabia ndio chanzo cha matendo tunayoyaona kama kukosekana kwa uaminifu, ubadhilifu wa mali za umma, ufisadi, migogoro ya ndoa, misuguano ya kijamii, chuki, upendo, ugaidi, unyanyapaa, ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kidini, changamoto za kimalezi na kadhalika. Yote haya yanaweza kuchambuliwa na kupatiwa majibu yake kwa kutumia sayansi ya tabia (saikolojia). Katika makala haya nitatoa mifano mifano kadhaa kuonesha namna sayansi ya tabia, inavyoweza kutumika kutatua matatizo yanayoikabili jamii. Elimu na Kujifunza Katik...