MASOMO YA MISA DOMINIKA YA 3 YA PASAKA MWAKA C WA KANISA.
DOMINIKA YA 3 YA PASAKA YA MWAKA C WA KANISA. MASOMO YA MISA- 01/05/2022. SOMO LA KWANZA. Mdo 5:27b-32, 40b-41 Kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio. Nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha wakawaacha waende zao. Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. WIMBO WA KATIKATI. Zab 30: 1, 3, 5, 10-12 Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwaf