Mwandishi: Sir. FELIX, KALISTI J. Copyright: ISS Africa Rais wa Tanzania Samia Suluhu anasema katika baadhi ya maeneo kwenye majukumu yake ya urais amesimamia vyema zaidi kuliko marais wengine wanaume waliomtangulia.Rais wa Tanzania alisema alikabiliwa na changamoto za kutoaminiwa katika siku zake za kwanza ofisini kwa sababu yeye ni mwanamke - jambo ambalo alilazimika kulishinda. Bi Samia alikuwa akizungumza kwenye kongamano katika mji mkuu wa Ghana Accra – ikiwa ni ziara yake ya kwanza Afrika Magharibi tangu aapishwe kuwa rais kufuatia kifo cha mtangulizi wake John Magufuli Machi 2021.“Ilikuwa vigumu sana kuwafanya watu wa Tanzania kuniamini. Kwamba naweza kuendesha nchi sawa na wanaume – hiyo ndiyo ilikuwa changamoto kubwa,” alisema wakati wa kikao kilichoandaliwa kama sehemu ya mkutano wa kila mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)."Katika kipindi cha mwaka mmoja nimeonyesha nguvu za wanawake, niliongoza nchi kama wanaume walivyofanya na katika mazingira mengine kwa ubo...