UCHAMBUZI WA BAJETI YA TAIFA 2022/2023.
Mtayarishaji ni Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo
(MNEC-Taifa).
Na kuhaririwa na Mwl. Mwangoka Emmanuel (Mwanafunzi-UDOM)
Hello! WATANZANIA.
Nawasalimu nyote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA.
KAZI IENDELEE
Kwa leo natamani kubadilishana mawazo nanyi hasa kwenye kipindi hiki Cha uchambuzi wa Bajeti ya Taifa 2022/2023.
Kiufupi kweli serikali iko kazini kwa ajili ya waTanzania sote.
HONGERENI SANA
Kwa maoni yangu, bajeti ni nzuri imeandaliwa kwa ajili ya wananchi hasa mkazo mkubwa ukiwa kwenye miundo mbinu ya barabara, madaraja, kilimo ambapo tayari Ni ongezeko la kutosha kutoka sh. bilioni 275 hadi 900.
Lakini pia, inaleta unafuu kwa wazazi kwa kuondoa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano hadi sita ambapo Sasa wanafunzi watasoma bila Ada kutoka shule ya msingi na sekondari. Lakini pia, ujenzi wa VETA kwa kila mkoa na wilaya, ongezeko la bajeti ya uvuvi na ufugaji, mwendelezo wa miradi yote ya mkakati kama Bwawa la Mwalimu Nyerere, SGR na n.k. Kimsingi ni bajeti ya kuwakomboa wananchi.
MAONI YANGU
ILI bajeti hii iweze kuwa ya maana sana na ya msingi kwa WATANZANIA na hasa wanyonge, yafuatayo yanaweza kuangaliwa:-
✓Usimamizi makini na wa kiwango cha juu wa rasilimali za Taifa ni muhimu sana ili matumizi au ujenzi wake ulingane na thamani ya fedha zinazotolewa. Tumeona miaka mingi hela zikitengwa na miradi kujengwa chini ya kiwango au kuchelewa kujengwa kiasi cha kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi Kama ilivyodhamira ya Serikali.
√Mfumo wa elimu yetu ufanyiwe marekebisho makubwa kuendana na mahitaji au mazingira ya sasa.
Pamoja na kufuta ada ya wanafunzi toka kidato cha tano na sita, bado mfumo wetu wa elimu ni wa kikoloni, kwani ni mfumo wa kuwandaa vijana kuzunguka maofisini kutafuta kazi badala ya kujiajiri au kujitegemea.
√Pamoja na kuongeza bajeti ya kilimo , tukijua kilimo ndio uti wa mgongo wa Mtanzania kwa zaidi ya asilimia 75 ya watanzania wanaishi vijijini wakitegemea kilimo, Taifa lina kila sababu ya kuondokana na kilimo cha jembe la mkono. Taifa linapaswa kuelekeza nguvu kubwa kwenye kilimo cha umwagiliaji ( combined harvest) ikiambatana na mikopo yenye riba nafuu kwa watu wote ambao wanaamua kujiunga na kilimo. Pia wakulima hawa wahakikishiwe masoko ya uhakika. Na hili swala la masoko litasaidia Taifa kuthibiti na kubadili mfumo na kutoka kwenye kuuza malighafi na kuanza kuongeza thamani ya mazao ya wakulima ili kuleta tija kwa wananchi, wakulima. Pia wajengewe viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, lasivyo Kilimo chetu hakitakuwa na manufaa kwani ni cha kujikimu kikitegemea mvua zaidi.
√Pia, kwenye Kilimo suala la Matrekta na viwatilifu:
Kama Taifa linataka kuondokana na kilimo cha jembe la mkono na kinachochangia kwa sehemu kubwa pato la Taifa (40%), likaanza mchakato wa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza matrekta na viwatilifu hapa hapa nchini.
√Tehama iende na kusambaa Tanzania nzima hasa mkazo ukiwa kuimarisha miundombinu ya vijijini ambako huduma hii ni adimu, imebaki mijini tu ambako ni watoto wa wenye uwezo ndio wanafaidi mfano: kuomba admission kwenye vyuo vikuu, mikopo toka bodi ya mikopo, ajira portal na mengineyo, imeleta ufa mkubwa kati ya watoto wanaosoma shule za kayumba na za mijini, kumekuwa na ufa mkubwa.
√Taifa mbali ya kuendelea kujenga miundo mbinu bora ya reli kwa Tanzania, ni vyema miundo mbinu ya reli iliyopo kama reli ya TAZARA, reli ya Kaskazini, reli ya Kati na hasa Tabora hadi Kigoma iimarishwe, na Taifa kupunguza kama sio kuachana na matumizi makubwa ya barabara kwa mizigo mikubwa. Mataifa mengi kiuchumi yamepiga hatua kwa kutegemea usafiri wa reli, maji n.k, badala yake Taifa letu mkazo wa kutumia hasa reli umepigwa kisogo.
Aidha, ujenzi wa reli hasa kwa mikoa yenye makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga ni muhimu.
√Mbali ya Serikali kutulilia mkazo ujenzi wa vyuo vya veta, iandae mazingira sahihi ya kuwakopesha kwa riba nafuu wahitimu wote ili ongezeko la vijana kujiajiri kuongezeka.
√Suala la uzalendo kwa Taifa ni kitu kisichoepukika kama tunataka Taifa linalojitambua hasa kwa kuimarisha miundombinu ya vijana wote wanaomaliza kidato cha sita, vyuo vya kati na vyuo vikuu vyote kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa muda wa mwaka mmoja na sio miezi mitatu kama ilivyo sasa ambapo naweza sema wanaenda kwa upendeleo, hasa ukijua mpango wa sasa wa serikali kipaumbele cha ajira ni kwa wale waliopitia JKT.
Taifa linaogopa gharama kubwa ya ujenzi wa makambi mengi kwa kila mkoa, tunaliharibu Taifa kwa mikono yetu wenyewe kwani hupelekea kukosekana kwa vijana wengi kutokwenda JKT.
√Viwanda:
Ili Taifa liweze kusonga na kupiga hatua kubwa za maendeleo, viwanda vikubwa vya mikakati ni muhimu kuliko kuwa na bajeti nzuri lakini pembejeo zote kutegemea nje kwa wafadhiri, au nchi rafiki mfano:
Kuwa na viwanda vingi na vikubwa vya mbolea ili kutosheleza mahitaji ya kilimo kuliko kutegemea mbolea toka nje ambayo mara nyingi inachelewa kufika au kutofika kabisa, ongezeko la bei ya mbolea isiyoendana na mazingira ya kwetu kwani mbolea nyingi hizi zimechangia uharibifu wa mazingira
√Nguo:
Taifa letu linatumia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni katika uagizaaji wa nguo toka nje. Ni vyema kama Taifa linalojitegemea likaanza mchakato wa ujenzi wa viwanda vikubwa vya nguo .mfano:
Zanzibar inatumia dola za kimarekani bilioni 3 kila mwaka kuagiza nguo toka nje.
√Suala la Utalii:
Mkazo mkubwa Taifa limewekeza sehemu kubwa moja ya ukanda wa Kaskazini kwa mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha, lakini kuna maeneo mengi ndani ya nchi hii ambako vivutio vya utalii viko vingi mnoo na hasa mikoa ya nyanda za juu kusini na kupelekea Taifa kupoteza hela nchi za kigeni kwa kutovitangaza vivutio vyote vilivyoko katika mikoa ya Mbeya Njombe, Iringa, Rukwa na Katavi. Ni vyema mkakati mpya ukaandaliwa na serikali kutangaza maeneo hayo yaliyodumazwa.
Ni vyema, tukafanya hamasa hata mashuleni na vyuoni kuanza kutembelea maeneo hayo kwa promotion ili kuasaidia kukuza uelewa na kutangaza vivutio vipya.
√Mtayarishaji ni Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo
(MNEC-Taifa).
Na kuhaririwa na Mwl. Mwangoka Emmanuel (Mwanafunzi-UDOM).
Thanks π
ReplyDelete#stay tune in KAJO MNJELU BLOG for everyday news and updates.
Delete