BURKINA FASO: MAAFISA WA JESHI WAMPINDUA KIONGOZI DAMIBA
Burkina Faso: Maafisa wa jeshi wampindua kiongozi Damiba
Kapteni wa jeshi Burkina Faso ametangaza katika televisheni ya taifa kwamba amempindua madarakani kiongozi wa jeshi Luteni Kanali Paul-Henri Damiba.
Ibrahim Traore ameeleza sababu ya kuidhinisha mapinduzi hayo ni kutokana na kushindwa kwa Luteni Kanali Damiba kukabiliana na waasi.
Kadhalika ametangaza kuwa mipaka imefungwa kwa muda usiojulikana na shughuli zote za kisiasa zimesimamishwa.
Wanajeshi wa Damiba waliipindua serikali iliochaguliwa mnamo Januari, wakiishutumu serikali kushindwa kudhibti mashambulio ya wapiganaji wenye itikadi kali za kiislamu.
Lakini utawala wake pia umeshindwa kuzima ghasia za wapiganaji jihadi hao. Jumatatu, wanajeshi 11 waliuawa walipokuwa wakisindikiza msururu wa magari ya raia kaskazini mwa nchi.
Mapema Ijumaa, Damiba aliomba nchi isalie na utulivu baada ya kusikika milio ya risasi katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu.
Comments
Post a Comment