TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 01.10.2022
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 01.10.2022
Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Luis Campos amesema klabu hiyo ilifanya makosa kwa kuwasajili fowadi wa Brazil Neymar, 30, na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, katika madirisha ya hivi majuzi ya uhamisho. (Mail)
Mbappe aliipatia PSG orodha ya wachezaji wanne wanaotaka kuhama msimu huu wa joto ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 24. (RMC Sport - in French)
Mshambulizi wa RB Leipzig Mfaransa Christopher Nkunku, 24, tayari amekamilisha uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na Chelsea kwa pauni milioni 52 katika dirisha lijalo la usajili. (Bild)
Mshambulizi wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 22, alifikiria kuhamia Liverpool katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, lakini khakufikiria uhamia Manchester United hata chembe.
Aston Villa inamchunguza meneja wa zamani wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino na mkufunzi wa Villarreal Unai Emery huku kukiwa na uvumi juu ya mustakabali wa Steven Gerrard. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Arsenal na Brazil Gabriel Jesus amesema anahitaji mabadiliko kutoka kwa mfumo wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City na sasa anajisikia "huru" kucheza chini ya Mikel Arteta.. (ESPN)
Tottenham inamfuatilia kwa karibu James Maddison wa Leicester City, huku kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 "anataka sana" kuhamia klabu hiyo ya kaskazini mwa London. (Football Insider)
Meneja mpya wa Chelsea Graham Potter yuko tayari kumpa winga wa Marekani Christian Pulisic, 24, nafasi ya kujidhihirisha Stamford Bridge kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake. (90min)
Potter hajafunga mlango kwa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku kurejea Chelsea baada ya muda wake wa mkopo na Inter Milan na anatarajiwa kufanya mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mwishoni mwa msimu huu. (ESPN)
Meneja wa Aston Villa Steven Gerrard amesema Douglas Luiz, 24, hajakaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo, na hivyo kuongeza nafasi ya Arsenal kumsajili kiungo huyo wa kati wa Brazil. (Sun)
Kiungo wa kati wa Juventus na Italia Manuel Locatelli anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A katika dirisha la uhamisho la Januari huku Arsenal wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Calciomercato - in Italian)
Kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, alikataa ofa kutoka kwa Manchester United na Liverpool msimu huu. (Sport - in Spanish)
Beki wa Ufaransa William Saliba hana haraka ya kusaini mkataba mpya na Arsenal, huku vilabu kadhaa vikiwa na hamu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Five Insider)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, bado yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Manchester United msimu ujao wa joto. (ESPN)
Chelsea imemjumuisha mkuu wa RB Leipzig Christopher Vivell miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuwa mkurugenzi wa ufundi Stamford Bridge. (Standard)
Real Madrid wanapanga kumpa mlinzi wao wa Brazil Eder Militao, 24, nyongeza ya kandarasi hadi 2028 pamoja na kipengele cha kutolewa cha euro 1bn kikiwemo kwenye mkataba huo. (Fabrizio Romano)
Comments
Post a Comment