FREEMAN MBOWE; MWANASIASA,MFANYABIASHARA NA MKULIMA ASIYE OGOPA HASARA
Miaka 64 iliyopita familia moja ya kitajiri mkoani Kilimanjaro ilipata mtoto wa mwisho wa kiume ikamuita "Freeman" kwa maana ya mtu huru. Jina lake na mazingira yake ya malezi na makuzi ndiyo kitu kinachovutia watu wengi kutaka kumfahamu zaidi.
1.Imewezekanaje mtoto wa familia ya akitajiri,ambayo ilikuwa na kila kitu cha muhimu anachohitaji binadamu yeyote na kuridhika navyo kuingia katika harakati ngumu na hatari?
Freeman alilelewa maisha ya kawaida sana kwa kusoma shule za vijijini Machame kama Rambo Primary Kolira Secondary school, Kibaha Secondary school na kidato cha tano na kidato cha sita akamalizia Ihungo high school
2.Familia nyingi zinasomesha watoto ili wapate kazi au fedha za Kujikimu ktk maisha yao,na wakisha pata vitu hivyo hujihesabia kuwa wameridhika ama hujiona kufanikiwa kimaisha.
Lakini ni tofauti na Freeman ambaye hakuridhishwa na utajiri wa kipekee wa familia yake,umaarufu wa biashara za Baba yake tangu enzi za mkoloni, ingali amezungukwa na masikini kila kona, anajiunga nao na kuamua kuanzisha vuguvugu la safari ya madaliko kupitia siasa.
3.Kama ilivyo kwa familia nyingi, kama Baba yako angekuwa ni mtu wa karibu na Rais na kutengeneza familia hizi mbili kuwa rafiki kiasi cha Rais Nyerere kukubali kuwa Baba wa ubatizo wa watoto wa Mzee Aikael Mbowe au Nyerere kumtuma Mzee Aikael Mbowe kwenda kutoa posa ya ndoa ya mtoto wake Makongoro Nyerere Mkuu wa Mkoa Rukwa wa Sasa) kwa niaba yake
Ingetarajiwa ukaribu wa Baba yako na viongozi wa nchi ungeathiri mlengo wa kisiasa kwa kutaka usaidiwe kuwa mwanasiasa kwa Jina la Baba yako kupitia Chama tawala. Tofauti na Freeman ambaye ukaribu wa Baba yake na Rais Julius Kambarage Nyerere haukumtamanisha au kuvutiwa na siasa za chama tawala kwa mseleleko wa jina na heshima ya Baba yake kwa Rais Nyerere.
4.Miaka ya Mwanzoni mwa 1980 baada ya kumaliza masomo Freeman Mbowe kuruta wa JKT kutoka Ruvu 32KJ na Lugalo kupitia operesheni Imarisha. 1982 aliajiriwa Benki Kuu kama Afisa wa Benki haikumfanya awe mtumwa wa ajira na kuona kama fadhila kutoka kwa chama tawala,aka acha kazi na kwenda kujitafutia maisha kwa kuanzisha biashara zake binafsi.
5.Miaka ya 1980 utajiri wa Familia ya Freeman Mbowe na Mohamed Dewji ulikuwa karibuni unalingana au Familia ya Freeman Mbowe ilikuwa tayari familia ya Wafanyabiashara wenye mafanikio zaidi kuliko ya Dewji.
6.Mwaka 1985 akiwa Kijana wa miaka 24 tu kupitia Idara ya Fedha za nje (foreign exchange) ya Benki Kuu tayari Freeman Mbowe alikuwa na exposure ya biashara ya Kimataifa, uthubutu na ubunifu wa hali ya Juu.
Aliamua kuacha Kazi Benki Kuu na kwenda kusoma akiwa tayari ana kampuni zake za biashara za kuingiza na kusafirisha bidhaa kupitia F&M Export Company LTD mwaka 1985 kampuni ya uvuvi wa samaki aina Kamba na Kamba kochi akiwa anamiliki boti moja ya kwake binafsi aina ya MV RSVP
Na baadae Freeman Mbowe akianza kupeleka Matunda nje ya nchi Kwa kutumia shirika la ndege la Gulf Air na baadae kuanzisha Kampuni ya "KILI VAGE" Kwa ajili ya kuuza Mbogamboga nje ya nchi.
7.Freeman Mbowe akiwa tayari mfanya biashara Mkubwa akaingia katika biashara ya majumba (Real estate) kwa kuingia ubia wa miaka 90 na Msajili wa Nyumba/ National Housing kwa kukiendeleza kiwanja namba 725 na 726/11 vya mtaa wa Mkwepu na Makunganya kwa asilimia 75 za Mbowe na 25 za National Housing palijulikana kama Club Billcanas.
Freeman Mbowe akajitanua na kununua nyumba za biashara ya kupangisha (apartments) London Uingereza,Nairobi Kenya, Johannesburg South Africa, Dubai na kumiliki na kuendesha Hotel ya Aishi Protea Hotel, Machame.
New Palace Hotel ilikuja kujulikana kama Mbowe Hotel
kwa sababu New palace Hotel alipatiwa Mzee Aikael Mbowe na serikali baada ya serikali kutaifisha kiwanja na Hotel yake ya SPLENDID HOTEL mali ya Mzee Aikael Mbowe iliyokuwa Mtaa wa Samora kwa sasa ndipo ilipo Twiga Banckorp
Katika Kujichanganya makundi mbali mbali ya Jamii, amewahi kuwa mfadhili wa Club ya Dar Young Africans (Yanga) kupitia biashara yake ya Club billcanas .
8.Freeman Mbowe akaonyesha uthubutu kuwa mtu binafsi na mfanyabiashara wa kwanza kuleta wanamuziki wa kutoka DR Congo kufanya maonyesho ya muziki kabla ya mtu yeyote.
9.Freeman Mbowe akiwa na miaka 29 tu akawa muasisi kijana wa CHADEMA, na akawa kijana wa kwanza kufanya kazi kubwa ya kuongoza "wing" ya vijana ndani ya CHADEMA
Mwaka 2004 baada ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA alianza kuwekeza nguvu na akili zake CHADEMA kwa kufanyia maboresho ya katiba, rangi Kadi, bendera, muundo wa CHADEMA kutoka mikononi kwa wazee wake Edwin Mtei na Bob Makani
10.Mwaka 2005 akiwa Mwenyekiti Kijana, akiwa na mwaka mmoja ofisini alilazimika kuingia katika kinyang'anyiro cha ugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mshindani wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Freeman Mbowe alipata idadi ya Kura 668,756 sawa na asilimia 5.88%,Wabunge watano wa majimbo na viti Maalum 6 (wabunge 11) na madiwani 103 lakini alifanikiwa kukitangaza sana chama chake cha CHADEMA na kukifanya kiwe midomoni mwa Watanzania
Staili yake ya pekee ya kutumia usafiri wa Helicopter na muasisi staili na aina hiyo katika kampeni za 2005 na vazi lake gwanda la kaki zilivutia sana na kumfanya yeye na CHADEMA kujulikana sana nchi nzima.
10.Kuanzia mwaka 2005 Freeman Mbowe amekuwa Kiongozi ,mfadhili na mwanamageuzi mkubwa wa kutafuta vijana wenye vipaji vya siasa kuwalea na kuwakuza. Mifano katika eneo hili ipo mingi sana na kujivunia.
John Mrema (UDSM), Zitto Kabwe (UDSM, Halima Mdee (UDSM), John Mnyika (TYVS), Benson Kigaila (UDP), Msafiri Mtemelwa (NCCR), Kitila Mkumbo (UDSM), David Kafulila (UDSM), David Silinde (UDSM), John Heche (SAUT), Juliana Shonza (UDSM), Joshua Nassari (UDSM), Salum Mwalimu (VODACOM), Boniface Jacob (UDSM), Deogratius Munisi (UDSM), Patrobas Katambi (SAUT), Godlisten Malisa (SAUT) Emmanuel Ntobi (NBC),Catherine Ruge (NBC),Vincent Mashinji (Chama cha Madaktari) na wengine wengi.
11.Freeman Mbowe amekuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa kuwavutia wanasiasa wengine kuhamia CHADEMA kutoka vyama vingine vya siasa. Wapo wanasiasa wengi walitoka katika vyama vyao na kuhamia CHADEMA na kuwa wanasiasa wakubwa na mahiri sana.
Dr. Aman Walid A. Kabourou (USA), Dr.Wilbroad Peter Slaa (CCM), Erasto Tumbo (UDP), Antony Komu (NCCR), Msafiri Mtemelwa (NCCR), Prof Mwesiga Baregu (NCCR), Tundu Lissu (NCCR), Prof Abdallah Safari (CUF), Mabere Nyaucho Marando (NCCR), Wilfred Lwakatare (NCCR), Godbless Lema (TLP), Ester Bulaya (CCM), Arcado Ntagazwa(CCM), Makongoro Mahanga (CCM),Razaro Nyalandu (CCM) PM-Frederick Sumaye (CCM),PM-Edward Lowasa (CCM).
12.Freeman moja ya sifa yake ni pale anapo ona kipaji cha mtu ktk siasa hana wivu wala haogopi kuwekeza kwake.
Alipomuhitaji Dr.Wilbroad Peter Slaa Kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuogopa Kumnunulia nyumba ya Kuishi Mbweni na kumtafutia gari aina ya Landcruiser V8 double exhaust,Diesel engine apige kazi nchi nzima kukuza na kuenezea CHADEMA.
Ukiondoa mwaka 2005 alipogombea yeye binafsi Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini chaguzi zingine 3 ametafuta na kushawishi wagombea Urais kwa ticket ya CHADEMA na Kuwekeza nguvu na fedha kwa wagombe wake katika michakato ya kampeni
Mwaka 2015 ukiondoa umashuhuri na ukubwa mgombea urais wa CHADEMA Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa aliyehamia CHADEMA tarehe 28 July 2015,ikiwa ni wiki mbili tu kabla ya kampeni.
Freeman alikuwa ameshajipanga kwa uchaguzi na kuagiza vifaa vya Kampeni kama vile bendera,Skafu,Vitambaa,Magari,Stage na PA system
za kampeni kutoka Guangzhou,China baada ya kuuza moja ya nyumba yake binafsi April 2015 ya nchini uingereza kupitia kampuni ya Artetra World Wide Limited yenye anuani S.L.P 293816 ktk Jengo la World Trade Center, Mtaa wa Sheikh Zayed,Dubai.
13.Pamoja na kukuza na vipaji vya vijana na kuwatengenezea mazingira mazuri vijana wadogo katika siasa za Tanzania. CCM imekuwa ikiwinda vijana wake na kuwachukua kwa ahadi ya kuwapa madaraka au fedha
Wengine Wamekuwa na shukrani za Punda pale wanapopata majina na umashuhuri huanza Kuona CHADEMA na Freeman Mbowe ni gunia la mazoezi la matusi na udhalilishaji kwa minajili ya kujitengenezea thamani kwa CCM wanapoamua kuhamia huko.
Pamoja na yote hayo Freeman Mbowe ni Mwanasiasa, mfanyabiashara na mkulima asiyeogopa hasara. Ameendelea kutengeneza vijana wengine kila siku bila kuchoka wala kujali kama ipo siku na wao wataondoka CHADEMA kwa matusi na kejeli kubwa kwake au CHADEMA.
Ukiwa mtu unayeogopa hasara huwezi kuwekeza katika biashara, ukiwa mtu unayehofia hasara huwezi kuwa mkulima, ukiwa unaogopa matusi na udhalilishaji huwezi kuwa mwanasiasa,mahiri, bora na mkubwa.
Comments
Post a Comment