Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na Watendaji wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu- ATS, leo Februari 11,2022 jijini Dodoma. Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu- ATS, Separatus Fella akielezea utendaji kazi wa Sekretarieti hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo Februari 11,2022 jijini Dodoma. Afisa wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu- ATS, Alex Lupilya akieleza changamoto zinazowakabili Sekretarieti hiyo wanapopambana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu nchini kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo Februari 11,2022 jijini Dodoma. .......................................................................... Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewataka Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Bin...