Mtayarishaji ni Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo (MNEC-Taifa). Na kuhaririwa na Mwl. Mwangoka Emmanuel (Mwanafunzi-UDOM) Hello! WATANZANIA. Nawasalimu nyote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA. KAZI IENDELEE Kwa leo natamani kubadilishana mawazo nanyi hasa kwenye kipindi hiki Cha uchambuzi wa Bajeti ya Taifa 2022/2023. Kiufupi kweli serikali iko kazini kwa ajili ya waTanzania sote. HONGERENI SANA Kwa maoni yangu, bajeti ni nzuri imeandaliwa kwa ajili ya wananchi hasa mkazo mkubwa ukiwa kwenye miundo mbinu ya barabara, madaraja, kilimo ambapo tayari Ni ongezeko la kutosha kutoka sh. bilioni 275 hadi 900. Lakini pia, inaleta unafuu kwa wazazi kwa kuondoa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano hadi sita ambapo Sasa wanafunzi watasoma bila Ada kutoka shule ya msingi na sekondari. Lakini pia, ujenzi wa VETA kwa kila mkoa na wilaya, ongezeko la bajeti ya uvuvi na ufugaji, mwendelezo wa miradi yote ya mkakati kama Bwawa la Mwalimu Nyerere, SGR na n.k. Kimsingi...