Posts

Showing posts from September, 2024

FREEMAN MBOWE; MWANASIASA,MFANYABIASHARA NA MKULIMA ASIYE OGOPA HASARA

Image
Miaka 64 iliyopita familia moja ya kitajiri mkoani Kilimanjaro ilipata mtoto wa mwisho wa kiume ikamuita "Freeman" kwa maana ya mtu huru. Jina lake na mazingira yake ya malezi na makuzi ndiyo kitu kinachovutia watu wengi kutaka kumfahamu zaidi. 1.Imewezekanaje mtoto wa familia ya akitajiri,ambayo ilikuwa na kila kitu cha muhimu anachohitaji binadamu yeyote na kuridhika navyo kuingia katika harakati ngumu na hatari? Freeman alilelewa maisha ya kawaida sana kwa kusoma shule za vijijini Machame kama Rambo Primary Kolira Secondary school, Kibaha Secondary school na kidato cha tano na kidato cha sita akamalizia Ihungo high school 2.Familia nyingi zinasomesha watoto ili wapate kazi au fedha za Kujikimu ktk maisha yao,na wakisha pata vitu hivyo hujihesabia kuwa wameridhika ama hujiona kufanikiwa kimaisha. Lakini ni tofauti na Freeman ambaye hakuridhishwa na utajiri wa kipekee wa familia yake,umaarufu wa biashara za Baba yake tangu enzi za mkoloni, ingali amezungukwa na masikini kila...