Posts

Showing posts from October, 2022

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 01.10.2022

Image
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 01.10.2022 CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Neymar na Mbappe KAJO MNJELU BLOG  Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Luis Campos amesema klabu hiyo ilifanya makosa kwa kuwasajili fowadi wa Brazil Neymar, 30, na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, katika madirisha ya hivi majuzi ya uhamisho. (Mail) Mbappe aliipatia PSG orodha ya wachezaji wanne wanaotaka kuhama msimu huu wa joto ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 24. (RMC Sport - in French) Mshambulizi wa RB Leipzig Mfaransa Christopher Nkunku, 24, tayari amekamilisha uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kujiunga na Chelsea kwa pauni milioni 52 katika dirisha lijalo la usajili. (Bild) Mshambulizi wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 22, alifikiria kuhamia Liverpool katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, lakini khakufikiria uhamia Manchester United  hata chembe.  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya...

BURKINA FASO: MAAFISA WA JESHI WAMPINDUA KIONGOZI DAMIBA

Image
Burkina Faso: Maafisa wa jeshi wampindua kiongozi Damiba CHANZO CHA PICHA, RADIO TELEVISION DU BURKINA Maelezo ya picha, Ibrahim Traore alitaja sababu ya kupinduliwa kwa Lt Kanali Damiba kutokana na kushindwa kukabiliana na waasi wa Kiislamu. Kapteni wa jeshi Burkina Faso ametangaza katika televisheni ya taifa kwamba amempindua madarakani  kiongozi wa jeshi Luteni  Kanali Paul-Henri Damiba. Ibrahim Traore ameeleza sababu ya kuidhinisha mapinduzi hayo ni kutokana na kushindwa kwa Luteni Kanali Damiba kukabiliana na waasi. Kadhalika ametangaza kuwa mipaka imefungwa kwa muda usiojulikana  na shughuli zote za kisiasa zimesimamishwa. Wanajeshi wa Damiba waliipindua serikali iliochaguliwa mnamo Januari, wakiishutumu serikali kushindwa kudhibti mashambulio ya wapiganaji wenye itikadi kali za kiislamu. Lakini utawala wake pia umeshindwa kuzima ghasia za wapiganaji jihadi hao. Jumatatu, wanajeshi 11 waliuawa walipokuwa wakisindikiza msururu wa magari ya raia  kaskazini mwa nc...